Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BALAA LA NJAA LANUKIA SUDAN KUSINI.

BALAA LA NJAA LANUKIA SUDAN KUSINI.

Written By Unknown on Friday, 4 July 2014 | Friday, July 04, 2014

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yametahadharisha kuwa baa la njaa linaweza kuikumba Sudan Kusini katika wiki kadhaa iwapo fedha hazitotolewa kwa ajili ya kufadhili misaada ya chakula.
Kamati ya Majanga ya Dharura ya Uingereza (DEC) ambayo ni muungano wa mashirika makubwa 13 ya misaada ikiwemo Oxfam imetahadharisha leo kuwa, iwapo mgogoro wa Sudan Kusini utaendelea na misaada kutopelekwa kwa wingi nchini humo, hadi kufikia Agosti mwaka huu baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanaweza kukumbwa na baa la njaa.

Ameongeza kuwa, DEC ina chini ya nusu ya fedha zinazohitajika kusaidia kupunguza mgogoro wa chakula Sudan Kusini ili usibadilike na kuwa janga. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa baa la njaa hutokea pale asilimia 20 ya familia zinapokuwa na uhaba wa chakula na asilimia 30 ya jumla ya watu wote kuwa na utapiamlo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi