Libya imesema kuwa serikali imedhibiti tena vituo viwili vya
kusafirishia mafuta katika Rasi ya Lanuf na al Sidra, ambavyo vilikuwa
vimetekwa na wanamgambo. Akizungumza katika mkutano wa waandishi habari
pamoja na kiongozi wa wanamgambo Ibrahim Jodhran, Waziri Mkuu wa
serikali ya mpito ya Libya Abdallah al Thani amesema kwamba, hivi sasa
vituo hivyo vinadhibitiwa na serikali na kwamba vimeanza tena kufanya
kazi.
Al Thani ameongeza kuwa, mgogoro wa mafuta nchini Libya sasa umemalizika baada ya kufikiwa makubaliano kati ya serikali na wanamgambo. Hata hivyo bado vituo vingine viwili vya mafuta vinakaliwa kwa mabavu na wanamgambo wa Libya. Wanamgmabo na makabila ya maeneo ya mashariki na magharibi mwa Libya ambako kuna utajiri mkubwa wa mafuta wanataka kupewa fungu kubwa zaidi la mapato ynayotokana na utajiri huo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!