Jeshi la Sudan limetangaza kuwa katika siku za usoni litaaza operesheni kubwa ya kijeshi katika maeneo yenye machafuko ili kuwatokomeza kabisa waasi. Msemaji wa jeshi la Sudan Sawarmi Khalid Sa'ad ameeleza kuwa, jeshi linaandaa mpango kwa ajili ya kuanza operesheni kubwa katika maeneo yenye machafuko ili kutokomeza kikamilifu makundi ya waasi.
Kwingineko serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa ipo tayari kufikia makubaliano ya amani na waasi, ikiwa ni baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuziwekea vikwazo pande hizo mbili. Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei ambaye pia ni msemaji rasmi ya tume ya mazungumo ya Juba amesema kuwa, muda wa siku 60 zilizowekwa na jumuiya ya IGAD unakwisha na serikali ipo tayari kutia saini makubaliano ya amani katika siku 15 zilizobakia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!