Klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid CF, imetajwa kuwa kinara katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa duniani kote.
Kwa mujibu wa orodha ya Forbes klabu ya Real Madrid imeonekana kileleni baada ya kubainika ina thamani ya takriban dola bilioni 3.44, ikifuatiwa na FC Barcelona iliyoshika nafasi ya pili, kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.2 na Manchester United inakamata nafasi ya tatu ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.81.
Klabu ya New York Yankees ya mchezo wa baseball ya nchini Marekani imeshika nafasi ya nne ikiwa na thamani ya dola bilioni 2.5. Nafasi ya tano inashikiliwa na Dallas Cowboys ya mchezo wa American Football ambayo ina thamani ya dola bilioni 2.3.
Forbes imetathmini thamani ya klabu hizo kwa kutazama thamani ya hisa, madeni na mikataba ya viwanja vyao

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!