TETESI ZA SOKA ULAYA.
Arsenal wamepata matumaini zaidi ya kumsajili Sami Khedira, 27, baada ya kiungo huyo kukataa kusaini mkataba mpya na Real Madrid (Daily Star), Arsenal pia wapo katika mazungumzo ya kumsajili Loic Remy kwa pauni milioni 8 kutoka QPR iliyopanda daraja (Independent), hata hivyo mazungumzo kati ya Arsenal na Remy yanadaiwa kuvunjika baada ya Remy kutokubali maslahi binafsi, huku Newcastle na Tottenham wakitaka kumchukua (Daily Mail), Chelsea wanataka pauni milioni 8 kwa ajili ya beki Ryan Bertrand, 24, ambaye ananyatiwa na Liverpool na Tottenham (Daily Express), mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Marouanne Chamakh, 30, amekubali mkataba wa miaka miwili kusalia Crystal Palace, huku akikubali kupunguziwa mshahara kiwango kikubwa (Guardian), Liverpool wameingia kwenye mbio sawa na Tottenham za kumsajili Wilfried Bony, 25, ambaye Swansea wanamuuza kwa pauni milioni 20 (Talksport), Lazio wanaamini wana kipaumbele zaidi kumsajili Stefan De Vrij, 22, kutoka Feyenoord, ambaye anasakwa pia na Manchester United (Daily Express), kiungo wa Spain Mikel Arteta, 32, hana nia ya kuhama Arsenal kwa mujibu wa wakala wake Inaki Ibanez (Times), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha usajili wa Javi Manquillo kutoka Spain na Mathieu Debuchy, kuziba nafasi za Bacary Sagna na Carl Jenkinson (Daily Mail), Everton huenda wakamsajili Muhamed Besic, 21, raia wa Bosnia Herzegovina kwa euro milioni tano (Daily Mirror), kiungo wa Juventus amezua gumzo zaidi la kuhamia Chelsea baada ya kuonekana katika mitaa ya Stamford Bridge (Daily Mail), Manchester United huenda wakamfuatilia Ben Davies kuziba nafasi ya Patrice Evra (Daily Mail), Chelsea wamejiunga na Arsenal na Liverpool kumwania mshambuliaji wa Real Sociedad Antoine Griezman, 23 aliyekataa mkataba mpya (Daily Express), mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, anatazamiwa kwenda Juventus kwa pauni milioni 17.5. Real Madrid watakuwa na uwezo wa kumnunua tena baada ya mwaka mmoja kwa pauni milioni 23.8 (Daily Mail). Hizo ndio tetesi za leo, share na wapenda soka wote. Nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!