Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HALI HII INATIA HURUMA,..WA PALESTINA WAPATAO 107 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA MASHAMBULIZI MAKALI YAKUVIZIA YA MAJESHI YA ISRAEL KWENYE UKANDA WA GHAZA.

HALI HII INATIA HURUMA,..WA PALESTINA WAPATAO 107 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA MASHAMBULIZI MAKALI YAKUVIZIA YA MAJESHI YA ISRAEL KWENYE UKANDA WA GHAZA.

Written By Unknown on Friday, 11 July 2014 | Friday, July 11, 2014

Utawala haramu wa Israel unaendeleza hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Ghaza ambapo idadi kubwa ya Wapalestina waliouawa shahidi ni wanawake na watoto. Hadi kufikia sasa idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika hujuma za ndege za kivita za utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo lililozingirwa la Ukanda wa Ghaza imeongezeka na kufika zaidi ya 107 na zaidi ya 700 kujeruhiwa. Ndege za utawala haramu wa Israel zimeshambulia maeneo 600 katika eneo hilo la Palestina katika kipindi cha siku tatu zilizopita. Imedokezwa kuwa utawala haramu wa Israel umewatayarisha askari 20,000 kuvamia Ghaza kupitia nchi kavu. Kufuatia tetesi hizo, Osama Hamdan mkuu wa kamati ya uhusiano wa kimataifa katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamams ameonya kuwa harakati hiyo itakabiliana vilivyo na vikosi vya Israel vikianzisha hujuma ya nchi kavu dhidi ya Ghaza. Afisa huyo wa Hamas ameongeza kuwa utawala haramu wa Israel umepata kiburi cha kutenda jinai dhidi ya Wapalestina kutokana na uungaji mkono wa Marekani. Harakati za mapambano Palestina zimejibu hujuma ya Israel kwa kuvurumisha makombora dhidi ya miji inayokaliwa kwa mabavu na Israel. Baadhi ya duru zinasema makombora kutoka Ghaza yamewaangamiza Wazayuni 25 na hivyo kueneza hofu na wahaka miongoni mwa Wazayuni. 


Picha hizi hapa za shambuliyo hilo:

 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi