Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi Marzieh Afkam
amelaani mashambulizi makubwa ya Israe katika Ukanda wa Ghaza. Bi
Marzieh Afkam amesema utawala wa Kizayuni umekuwa ukiendesha
mashambulizi ya anga dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza tangu wiki mbili
zilizopita kwa kisingizio cha kutekwa nyara vijana watatu walowezi wa
Kiyahudi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa,
kuuliwa kikatili na Wazayuni kijana wa Kipalestina hivi karibuni huko
Quds ya Mashariki kunakumbusha hujuma zinazoendelea kufanywa na magaidi
huko Syria na Iraq na kwamba kunaonyesha namna utawala wa Kizayuni
usivyoweza kukabiliana na muqawama wa wananchi wa Palestina.
Bi Marzieh Afkam amesifu muqawama wa raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza dhidi ya mashambulizi ya Israel na kuzitolewa wito nchi za Kiarabu na Kiislamu na pia taasisi na makundi ya kutetea haki za binadamu kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya mauaji na jinai za utawala wa Kizayuni.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!