Gazeti moja la nchini Libya limeandika kuwa, kundi la magaidi wa
kitakfiri wa Daesh linajaribu kila linalowezekana ili kujipenyeza huko
Libya na kupanua maovu yake nchini humo. Gazeti la Buabatul Wasat
limeandika kuwa, maafisa wa idara za kiintelijenisia za Tunisia, Misri
na Algeria walikutana juma hili ili kuchunguza ripoti za kiusalama na
kutafuta njia za kuzuia kuenea kwa harakati za kigaidi za kundi la Daesh
katika eneo.
Gazeti hilo limevinukuu vyombo vya kiusalama na kuandika kuwa tetesi zilizopo zinaonyesha kuwa, baadhi ya Walibya wenye misimamo ya kufurutu ada wanarejea nchini humo na kujaribu kuasisi kambi kwa ajili ya kundi la Daesh huko kaskazini mwa Afrika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kukosekana serikali kuu yenye nguvu huko Libya tangu kung’olewa madarakani dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011 huenda kukaandaa mazingira ya kupanuka kwa harakati za kundi la kitakfiri la Daesh nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!