Shirika la Afya Duniani WHO limeripoti kuwa idadi ya watu waliofariki
dunia kwa homa ya ebola huko magharibi mwa Afrika imefikia 518. WHO
ilieleza jana Jumanne kuwa, kesi mpya 50 za homa ya ebola zimeripotiwa
kugunduliwa huko Guinea, Liberia na Sierra Leone kuanzia Julai 3 hadi 6.
WHO pia imeashiria kuwa, watu wengine 844 wanashukiwa kuambukizwa homa hiyo ya ebola. Guinea ni nchi ya magharibi mwa Afrika iliyoathiriwa vibaya na homa ya ebola ikiwa na watu 408 walioambukizwa homa hiyo huku wengine 307 wakiwa tayari wameaga dunia. Hadi sasa hakuna tiba ya ebola, homa ambayo dalili zake ni kutapika, kuharisha na kuvuja damu.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!