Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULIBAHATIKA KUYAONA YALE MABAO YOTE 7 YA UJERUMANI WALIYO WAJAZA WA BRAZIL?KAMA HUKUYAONA BASI HAYA HAPA.(PICHA)

JE,ULIBAHATIKA KUYAONA YALE MABAO YOTE 7 YA UJERUMANI WALIYO WAJAZA WA BRAZIL?KAMA HUKUYAONA BASI HAYA HAPA.(PICHA)

Written By Unknown on Wednesday, 9 July 2014 | Wednesday, July 09, 2014

UJERUMANI imetinga Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte, Brazil.
 No way back: Oscar and Fred stand ready at the centre circle with little hope of getting back into the game
Ujerumani inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12- mara ya mwisho ilifungwa na Brazil katika fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na Korea Kusini na Japan na sasa watamsubiri mshindi wa kesho kati ya Argentina na Uholanzi.
Hadi mapumziko, tayari Ujerumani walikuwa mbele kwa mabao 5-0 yaliyofungwa na Toni Kroos mawili, Miroslav Klose, Thomas Muller na Sami Khedira. Brazil ilionekana wazi kuathiriwa na pengo la kuwakosa wachezaji wake tegemeo, beki na Nahodha Thiago Silva anayetumikia adhabu ya kadi za njano na mshambuliaji Neymar ambaye ni majeruhi, ambao nafasi zao zilizibwa na Bernard na Dante.
Historic: The strike that made hm the record holder 
Ujerumani ilipata bao lake la kwanza dakika ya 11, mfungaji Thomas Mullerbaada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Brazil.Miroslav Klose akafunga la pili dakika 23 baada ya kuukuta mpira uliopanguliwa na kipa Julio Cesar kufuatia shuti lake mwenyewe na kuandika bao lake la 16 kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye fainali hizo, akimpiku Mbrazil, Ronaldo Lima.
 Disbelief: Fernandinho, Maicon and David Luiz look bemused following Germany's fifth goal of the evening
Toni Kroos akaifungia Ujerumani bao la tatu na la nne dakika za 24 na 26,kabla ya Sami Khedira kufunga la tano dakika ya 29. 
Kipindi cha pili, kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari alianza na mabadiliko, akiwatoa Fernandinho na Hulk na kuwaingiza Paulinho na Ramires, wakati mwenzake wa Ujerumani, Joachim Loew alimpumzisha Hummels na kumuingiza Mertesacker.
 Too easy! Eight Brazilians stand in the box as Muller finds space to guide the ball goalwards
Mabadiliko hayo kidogo yaliiongezea uhai Brazil na kupeleka mashambulizi langoni mwa Ujerumani, lakini wakaishia tu kukosa mabao ya wazi.
Ujerumani ikafunguka tena na kwenda kufunga mabao mawili zaidi, yote Andre
Schurrle aliyeingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Klose akimtungua kipa Julio Cesar dakika ya 69 na 79.  
Running riot: Germany scored four goals in six first-half minutes during Tuesday's semi-final against Brazil

Brazil ilianya tena mabadiliko, Fred akimpoisha Willian dakika ya 69, wakati
Ujerumani nayo ilimpumzisha Khedira nafasi yake ikachukuliwa na 
Draxler dakika ya 76.
Mesut Ozil alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 89, lakini akapiga nje na Brazil wakafanya shambulizi na kushitukiza na kujipatia bao la kufutia machozi lililofungwa na Oscar dakika ya 90. Wachezaji na mashabiki wa Brazil waliangua vilio baada ya mchezo huo, huku Wajerumani wakiangusha pati la maana uwanjani

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi