Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, ameanza
kujifua rasmi jana kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao lakini hapohapo
akamtupia dongo kiungo mpya wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.
Tambwe alitua nchini juzi usiku na kuamua kuingia mzigoni moja kwa
moja kujumuika na wenzake kwenye mazoezi ya gym yanayofanyika
huko Chang’ombe, ni Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Tambwe alisema kuwa alirejea
kuendelea na makali yake na yupo fiti kwa ajili ya msimu ujao lakini
akaongeza kwamba, hahofii ujio wa mchezaji Coutinho kwa kuwa anaamini atakuwa na
kiwango cha kawaida.
“Kwani Brazil kitu gani, unaweza ukatoka Brazil na ukawa wa kawaida
tu, mimi simjui na sijawahi kumuona lakini hawezi kusumbua kichwa kwa
sababu si wote wanaotoka Brazil wanajua mpira, cha msingi kama kweli ni
mzuri basi tutamuona uwanjani.
“Kama ingekuwa kila Mbrazili ni mzuri na wanajua mpira kuliko wengine wote basi wasingefungwa 7-1 na Ujerumani,” alisema Tambwe.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!