Hatimae washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal,
wamethibitisha taarifa za kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji
kutoka nchini Chile na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Alexis
Alejandro Sánchez.
Arsenal wamethibitisha kukamilishwa kwa dili la usajili wa mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 25, usiku wa kuamki hii leo baada ya kumfanyia vipimo vya afya huko jijini London.
Usajili wa mshambuliaji huyo ambaye aliitumikia nchi yake katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, ambazo zitafikia tamati mwishoni mwa juma hili huko nchini Brazil, umeigharimu The Gunners kiasi cha paund million 35.
FC Barcelona wamekubali kumuachia Alexis Alejandro Sánchez baada ya kuwa na matumaini ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Uruguay pamoja na klabu ya Liverpool Luis Alberto Suarez Diaz ambaye usajili wake utaigharimu klabu hiyo ya Cataluña zaidi ya paund million 70.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!