Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA NIGERIA ZASEMA KUWA MJI WA BUNI YADI WA KASKAZINI MWA NCHI HIYO UMETEKWA NA KUNDI LA BOKO HARAM

HABARI KUTOKA NIGERIA ZASEMA KUWA MJI WA BUNI YADI WA KASKAZINI MWA NCHI HIYO UMETEKWA NA KUNDI LA BOKO HARAM

Written By Unknown on Friday, 22 August 2014 | Friday, August 22, 2014

Kundi la kitakfiri la Boko Haram limeuteka mji wa Buni Yadi katika jimbo la Yobe huko kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Msemaji wa Gavana wa jimbo hilo Ibrahim Geidam amethibitisha kwamba mji huo umetekwa na waasi wa kundi la Boko Haram na kusisitiza kuwa, wakazi wengi wa mji wa Buni Yadi wameukimbia mji huo. Amesema kundi hilo limekuwa likiua raia katika eneo hilo na kupora mali zao.

Kundi hilo linalaumiwa kwa kuua ovyo raia wa kawaida. Mwezi Februari mwaka huu wanachama wa kundi hilo waliua makumi ya wanafunzi katika shule moja kwenye mji huo huo wa Buni Yadi. Aprili mwaka huu pia wapiganaji wa Boko Haram waliwateka nyama mamia ya wanafunzi wa kike katika mji wa Chibok na kuwapeleka kusikojulikana. Inakadiriwa kuwa kundi hilo limeua zaidi ya watu elfu kumi tangu lilipoanza kushambua maeneo mbalimbali ya Nigeria mwaka 2009.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi