Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » JE,ULIJUWA SABABU ZILIZO MPELEKEA BALOTELLI KUAMUWA KUVAA JEZI YENYE NAMBA 45 KWENYE CLUB YA LIVERPOOL?

JE,ULIJUWA SABABU ZILIZO MPELEKEA BALOTELLI KUAMUWA KUVAA JEZI YENYE NAMBA 45 KWENYE CLUB YA LIVERPOOL?

Written By Unknown on Wednesday, 27 August 2014 | Wednesday, August 27, 2014

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Liverpool, Super Mario Barwuah Balotelli kwa mara ya kwanza ameeleza sababu ya kwa nini anapenda kuvaa jezi namba 45 tangu akiwa na umri mdogo mpaka sasa.
Balotelli, ambaye usiku wa kuamkia hii leo alikamilisha ndoto za kurejea tena nchini Uingeereza, baada ya kuwepo nchini humo miaka mitatu iliyopita akiwa na klabu bingwa Man City amesema wakati anajifunza soka kwenye klabu ya Inter Milan alitamani kuvaa jezi namba 9, lakini ilishindikana kutokana na vijana wote klabuni hapo kupewa nafasi ya kuwa na jezi kuanzia namba na thelathini mpaka hamsini na ushee.
Amesema sababu hiyo ilimnyima nafasi ya kufikia malengo aliyokuwa amejiwekea ya kuvaa jezi yenye namba anayoipenda, na ilifikiwa wakati alijituma kiakili kwa kufikiria ni vipi ataweza kulimaliza tatizo hilo ambalo halikuwa rahisi kutatuliwa kutokana na umri wake klabini hapo.
Amesema siku moja alipata ufumbuzi kwa kuamini atatimiza ndoto za kuvaa jezi namba tisa kwa ubunifu, na ndipo alifanya maamuzi ya kuchagua jezi namba 45, ambapo kimahesabu namba nne ukijumlisha na tano unapata namba tisa.
“Siwakuwa na furaha kutokana na changamoto hiyo ambayo ilikuwa inanihangaisha kila siku, lakini kuna siku nilikamilisha ndoto zangu kwa kufanikiwa kuvumbua ubinifu wangu wa kuamini nitavaa jezi namba tisa kwa kujiaminisha ili niweze kucheza soka sawa sawa” Amesema Balotelli
Kutokana na ubunifu huo Balotelli amesema alijihisi furaha na aliendelea kutimiza wajibu wake alipokuwa uwanjani na kila mara alifanikiwa kufunga mabao mengi na kujipongeza kwa kuamini namba tisa iliyopo mgogoni mwake ndio chagizo la kufanikisha alichokiwaza siku zote.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi