Mchezaji bora wa soka barani Ulaya Cristiano Ronaldo dos Santos
Aveiro amemtakia kila la kheri mshambuliaji mpya wa klabu ya Man Utd
Ángel Fabián Di María Hernández katika majukumu yake akiwa Old Trafford
huko nchini Uingereza.
Ronaldo ambaye alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa barani Ulaya jana jioni kwa kuwashinda wapinzani wake Manuel Neuer pamoja na Arjen Robben amesema anatambua uwajibikaji wa Di Maria unaweza kufanya mageuzi makubwa katika kikosi cha Man Utd.

Lakini pamoja na kumtumia salamu za kumtakia kheri Ronaldo amemtaka
Di Maria kuitendea mema jezi namba saba aliyokabidhiwa kwa kumueleza
kwamba jezi hiyo ina majukumu makubwa.
Amesema wakati akisajiliwa Man utd mwaka 2003 alikabidhiwa jezi namba
saba ambayo ulikuwa inatumiwa na gwiji wa soka nchini Uingereza David
Robert Joseph Beckham na bila ajizi aliitendea mema kwa kufanya kusudio
la kuibeba Man Utd wakati wote.
Hata hivyo Di Maria amekiri ni kweli alielezwa maneno hayo na Ronaldo
na ameahidi kufanya jitihada za kutimiza kusudio la kuirejeshea fadhila
jezi namba saba ya Man Utd.
Di Maria alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari hapo jana.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!