Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIKI NDICHO KILICHO MFANYA KOCHA WA EVERTON AMSAJILI MUAFRIKA SAMUEL ETO'O.

KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI HIKI NDICHO KILICHO MFANYA KOCHA WA EVERTON AMSAJILI MUAFRIKA SAMUEL ETO'O.

Written By Unknown on Thursday, 28 August 2014 | Thursday, August 28, 2014

Mshambuliaji kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Cameroon Samuel Eto'o Fils ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Everton kwa mkataba wa miaka miwili.
Meneja wa klabu ya Everton Roberto Martínez Montoliú amemtambulisha Eto’o mbele ya waandishi wa habari pamoja na kutoa sababu za kile kilichomvutia kumsajili mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliitumikia Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Martinez amesema uwajibikaji na kujituma kwa mshambuliaji huyo kutoka nyumbani Afrika ndio chagizo kubwa lililompa msukumo wa kumsajili baada ya kuona uwezekano wa kuwa nae kwenye kikosi cha The Toffees.
Amesema kabla ya kukamilisha mipango ya kumsaili aliketi kitini na Samuel Eto’o na kumueleza nini anachokihitaji kutoka kwake na mwishowe walifikia makubaliano ya kiutendaji, hali ambayo anaamini aitakamilishwa kwa vitendo uwanjani.

 
Samuel Eto’o anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Everton ambacho mwishoni mwa juma hili kitapambana na Chelsea kwenye uwanja wa Goodson Park huko jijini Liverpool.

 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi