Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MANCHESTER UNITED YAINGIA VITANI NA WAPIGA BUNDUKI AMBAO NI ARSENAL WAKIKIPIGANIA HICHI KIFAA KUTOKA URENO.

MANCHESTER UNITED YAINGIA VITANI NA WAPIGA BUNDUKI AMBAO NI ARSENAL WAKIKIPIGANIA HICHI KIFAA KUTOKA URENO.

Written By Unknown on Thursday 28 August 2014 | Thursday, August 28, 2014

Katika kuhitaji kujiimarisha kabla ya dirisha la usajili halijafungwa usiku wa manane siku ya jumapili, Man Utd wamejikuta wakiingia vitani na wapinzani wao Arsenal kwenye mipango ya kumuwania kiungo mkabaji kutoka nchini Ureno na klabu ya Sporting Lisbon William Carvalho.
Man Utd wameingia katika vita hiyo ikiwa ni awamu yao ya pili kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, lakini kati kati ya mwezi uliopita walijiondoa na kuipisha Arsenal ambayo ilitajwa kuwa na mipango ya kumpeleka nchini Uingereza.
Man Utd wameonyesha lengo hilo kwa mara ya pili huku uongozi wa klabu ya Sporting Lisbon ukiwa umeshawaarifu Arsenal kutoa kiasi cha paund million 24, ili waweze kukamilisha dili hilo.
Hata hivyo bado haijafahamika kama klabu hizo za nchini Uingereza zimeshatuma ofa mjini Lisbon kwa ajili ya kuanza vita ya kumuwania William Carvalho ama la.
Carvalho alionyesha kiwango kizuri wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zilifanyika nchini Brazil, japokuwa timu yake ya taifa ya Ureno iliondolewa mapema katika hatua ya makundi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

1 comment:

  1. Mystino | online casino in Japan
    Mystino is the online casino that takes players to virtual worlds. If you have ever fun88 soikeotot visited the online casino then you william hill will undoubtedly know of it! There ミスティーノ are a number of

    ReplyDelete

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi