Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA ULIKUWA HUNA HABARI BASI HUYU NDIE MCHEZAJI WA TIMU YA ARSENAL ALIYE TANGAZA KUACHANA NA UVUTAJI SIGARA.

KAMA ULIKUWA HUNA HABARI BASI HUYU NDIE MCHEZAJI WA TIMU YA ARSENAL ALIYE TANGAZA KUACHANA NA UVUTAJI SIGARA.

Written By Unknown on Friday, 1 August 2014 | Friday, August 01, 2014

Kiungo kutoka nchini Uingereza Jack Andrew Garry Wilshere amewataka radhi mashabiki wa soka ulimwenguni kote ambao walichukizwa na kitendo cha uvutaji wa sigara ambacho alikionyesha akiwa mapumzikoni mjini Las Vegas, nchini Marekani.
Wilshire amefanya hivyo kwa kuamini hakuna hata mmoja kati ya mashabiki wake alifurahishwa na aliyoyafanya akiwa mapumzikoni, hali ambayo amekiri imemsikitisha hata yeye.
Amesema kinachotakiwa kwa sasa ni watu waka kumsamehe kwa kutambua yeye bado ni mtoto mdogo na anastahili kuelekezwa pale anapokosea.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, amesisitiza kuacha kabisa tabia ya uvutaji wa sigara na kuahidi kurejea katika maadili yaliyo mema na ikiwezekana kuonyesha uwezo mkubwa anapokuwa uwnajani kuanzia msimu ujao wa ligi.Wilshere alionekana akipuliza moshi akiwa sambamba na mlinda mlango wa Man City Joe Hart kupitia picha za mitandao ya kijamii, hali ambayo ilimpa kigugumizi meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kujibu tuhuma hizo alipoulizwa na vyombo vya habari na badala yake aliahidi kuzungumza na Jack atakaporejea kambini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi