Nijel Amos huyu ndo Bingwa wa dunia kwa sasa. |
Rudisha ambaye alikwenda nchini humo na matumaini makubwa ya kushikilia rekodi ya kuendeleza ubabe wa kutwaa medali ya dhahabu, alijikuta akishindwa kufurukuta baada ya kuzidiwa maarifa na mshiriki kutoka nchini Botswana Nijel Amos.
Amos, mwenye umri wa miaka 20 alkioneka kuwa makini zaidi ya Rudisha wakati wa mpambano wa mbio za mita 800, na hivyo aliandika historia ya kuwa bingwa wa michuano ya Jumuia ya madola kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo Amos, alianza kuonyesha ana uwezo wa kushindana na miamba mikubwa dunaini kama David Rudisha, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya Olympic ya mwaka 2012 iliyofanyika jijini London nchini Uingereza.
Hapo Amos akimuacha Rudisha...tazama vile Rudisha anavyo mtizama Amos |
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!