Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » HUYU NDO MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANII ANAE KABILIWA KWA NA HALI NGUMU BAADA YA KUTOKA JELA.

HUYU NDO MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANII ANAE KABILIWA KWA NA HALI NGUMU BAADA YA KUTOKA JELA.

Written By Unknown on Wednesday, 30 July 2014 | Wednesday, July 30, 2014

Mwimbaji wa Loyal, Chris Brown ambaye alitoka jela hivi karibuni na kuamua kutafuta amani kwa kuhama nyumba aliyokuwa akiishi kukwepa ugomvi na majirani zake ni kama ameruka majivu na kukanyaga moto.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo aliamua kuuza nyumba yake ya kifahari iliyokuwa Hollywood Hills kufuatia ugomvi wa kila siku na majirani zake waliomfikisha kwenye vyombo vya sheria mara kadhaa kwa madai ya kuwanyima raha na familia zao kwa vitendo vyake. Baada ya kuuza nyumba hiyo alinunua nyumba mpya, California.
Kwa bahati mbaya majirani wapya wa mwimbaji huyo wanaonekana kuwa na maamuzi magumu zaidi ya wale wa awali waliokuwa wanampeleka kwenye vyombo vya sheria.
Akiongea na TMZ, jirani mmoja alieleza kutofurahishwa kwake na ujio wa Chris Brown kwenye ujirani wao na kuahidi kuwa endapo atagusa nyumbani kwake atampiga risasi.
“It can be the devil. I can care less.. I don’t care if they are having orgies. It can even be Sadam Hussein for all I care, as long as he doesn’t trespass onto my property. If he does, I shoot him.”
Jumba jipya la Chris Brown lina vitu vya kifahari kama uwanja wa kuchezea tennis, dance studio, club house, commercial ice cream bar na mengine mengi huku eneo zima likuwa na ukubwa wa eneo la mraba futi 8,000 na vyumba sita vya kulala.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi