Shirika la Msamaha Duniani Amnesty
International limesema kuwa Marekani kwanza inapaswa kutilia maanani
ukiukaji wake wa haki za binadamu katika maandamano ya raia
yanayoendelea kufanywa huko Ferguson kabla ya kutoa tamko lolote kuhusu
miamala ya nchi nyingine. Katika hali ambayo maaandamo yanaendelea huko
Ferguson Marekani, Amnesty International imetangaza kuwa, Marekani
inapaswa kusafisha rekodi yake ya haki za binadamu na kuifuatilia kwa
makini kabla ya kuzungumza chochote kuhusu masuala ya haki za binadamu
katika nchi nyingine.
Amnesty International imetoa radiamali
hiyo huku wanaharakati wa kuteteta haki za binadamu katika maeneo
mbalimbali duniani wakikosoa vikali hatua ya polisi wa Ferguson ya
kutumia nguvu na silaha ili kuyakandamiza maandamano ya raia wa Marekani
wanaolalamikia vitendo vya kibaguzi huko Missouri baada ya polisi
kumuuwa kwa risasi kijana mmoja Mmarekani mweusi kwa jina la Michael
Brown ambaye alikuwa hana silaha yoyote.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!