Rapper Meek Mill ameendelea kusota gerezani huku matarajio yake ya kuachiwa Jumatatu ijayo yakotoweka baada ya jaji aliyemhukumu kifungo hicho kutoa amri ya kuendelea kubaki lupango.
Jaji huyo ameeleza kuwa anataka Meek Mill ahudhurie matibabu ya kudhibiti hasira pamoja na mafunzo maalum. Amesema alitaka rapper huyo mwenye umri wa miaka 27 awe na uwezo wa kukua na kufanya maendelea katika kazi ya muziiki lakini hawezi kufanya hivyo wakati ambapo anamuonesha dharau.
“I wanted him to be able to grow and get to the next level (of his career). But I can't do that with him thumbing his nose at me.” Jaji Genese Brinkley amekaririwa na Associated Press.
Meek Mill anashikiliwa kwa kosa la kuvunja masharti ya kifungo cha nje na tangu mwaka 2009 amekuwa chini ya kipindi cha matazimio kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya na bunduki kinyume cha sheria.
Kutokana na kuongezwa kwa muda huo, Meek Mill ataonekana uraiani October mwaka huu badala ya Jumatatu ijayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!