Beki wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Bacary Sagna, hatimae
amefichua siri nzito iliyokuwa imejificha moyoni mwake, baada ya
kuikacha klabu ya Arsenal na kukubali kujiunga na Man City.
Sagna, amelazimika kufichua siri hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Man City ambayo aliwahi kuikana kwa kusema haikuwa kwenye mawazo yake mara tu, alipokataa kusaini mkataba mpya na Arsenal.
Beki huyo ambaye ameondoka kaskazini mwa jijini London akiwa sehemu ya kikosi kilichorejesha heshima kwa kutwaa ubingwa wa kombe la FA msimu uliopita, amesema sababu kubwa ya kujiunga na mabingwa hao wa nchini Uingereza ni ushawishi alioupata kutoka kwa Samir Nasri pamoja na Gael Clichy.
Amesema kwa kipindi kirefu tangu wachezjai hao wawili walipoihama Arsenal, amekuwa akiwasiliana nao katika masuala yanayohusu maisha pamoja na urafiki uliopo baina yao, lakini miezi kadhaa iliyopita mazungumzo yao yalihamia kwenye ushawishi wa kumtaka ajiunge nao kwenye klabu ya Man city.
“Nilizungumza nao [Nasri na Clichy], mara nyingi zaidi na walinihakikishia uwezekano wa kusajiliwa kwenye klabu hii, na waliniambia mazingira yaliopo hapa, hivyo nilifanya maamuzi ya kujiunga na Man city.”
"Walijua mkataba wangu na Arsenal unamalizika mwishoni mwa msimu uliopita, hivyo waliitumia nafasi hiyo kunishawishi kwa usiku na mchana”.
"Wachezaji walio hapa wanajitahidui kufanya kazi kwa bidii ili wakamilishe malengo ya kutwaa vikombe kadhaa kila msimu, hivyo nimeona na mimi niwe sehemu yao.'
"Nimeitumikia Arsenal kwa kipindi cha miaka saba iliyopita na mengi mazuri yalikuwepo kwenye klabu hiyo mpaka kufikia hatua ya kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa FA msimu uliopita, na sasa ni wakati mzuri kwangu kuanza mwanzo nikiwa na klabu mpya”.
"Kwangu, Man City ni klabu kubwa, na sina budi kuitumikia kwa moyo wangu wote kutokana na malengo niliyoyakuta hapa.” Amesema Sagna mwenye umri wa miaka 31
Bacary Sagna ameondoka Arsenal huku akiacha kumbukumbu ya kucheza michezo 213 na kufunga mabao manne tangu mwaka 2007 aliposajiliwa na klabu hiyo ya Emitares Stadium, akitokea nyumbani kwao Ufaransa kwenye klabu ya Auxerre.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!