Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SIRI ZA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA ZAANZA KUTOBOLEWA,KAMISHNA WA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA U.N AWEKA MAMBO WAZI.

SIRI ZA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA ZAANZA KUTOBOLEWA,KAMISHNA WA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA U.N AWEKA MAMBO WAZI.

Written By Unknown on Friday, 22 August 2014 | Friday, August 22, 2014

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amelikosoa vikali Baraza la Usalama la umoja huo akisema limeshindwa kuchukua maamuzi muhimu ya kusitisha machafuko kwa sababu ya kulinda maslahi ya baadhi ya nchi.
Navi Pillay ambaye ataacha wadhifa huo siku chache zijazo, amesema msimamo na jibu kali zaidi la Baraza la Usalama linaweza kuokoa maisha ya mamia ya watu. Amekosoa vikali utumiaji wa kura ya veto na amezitaka nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama kuboresha maana ya maslahi ya kitaifa.
Matamshi hayo ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja yametolewa katika kipindi ambacho utumiaji wa kura ya veto umezusha mpasuko mkubwa kati ya nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ambazo zinatumia haki hiyo kukwamisha maamuzi ya kimataifa.

Hivi karibuni Marekani ilitumia kura hiyo kukwamisha maamuzi ya kimataifa ya kulaani mauaji ya kinyama ya Israel katika Ukanda wa Ghaza.
Siku chache zilizopita pia Navi Pillay aliyataja mauaji hayo kuwa ni jinai za kivita. Vilevile mwanadiplomasia huyo wa Afrika Kusini alilaani sera za kibaguzi za Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika kufuatia ghasia zinazoendelea katika mji wa Ferguson baada ya polisi ya Marekani kumpiga risasi na kumuua kijana Michael Brown ambaye hakuwa na silaha ya aina yoyote. Pillay ameifananisha hali ya sasa ya mji huo na ile iliyokuwapo nchini Afrika Kusini wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi na ameitaka serikali ya Marekani kufanyia kazi ukatili wa polisi na kuchunguza sababu za kimsingi za ubaguzi katika jamii ya Marekani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi