Ikiwa ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa
huo kupitia mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi
hizo kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki michuano
yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.
CAF itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia
katikati ya Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa
ajili ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa
kuruhusu au kuendelea kusimamisha.
Pia kutokana na mapendekezo
ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema kwa nchi zenye virusi vya Ebola
ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara
wa timu zao ili kuhakikisha wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!