Kampuni ya Apple imezindua bidhaa mpya ya saa za mkononi ya kisasa ‘smart watch’ inayoitwa iwatch ikiwa ni bidhaa ya kwanza kutambulishwa na kampuni hiyo tangu alipofariki muanzilishi wa kampuni hiyo, Steve Jobs.
Saa hiyo imetajwa kuwa na matumizi mengi kwa mtumiaji wa kisasa anaendana na teknolojia huku ikimrahisishia maisha kwa kiasi kikubwa hasa katika kufahamu kinachoendelea duniani na afya yake.
Saa hiyo ya iwatch ina uwezo wa kumonitor mapigo ya moyo ya mtumiaji na hali yake ya afya na kumtumia maelezo sahihi huku ikimchorea taswira ya shughuli mbalimbali anazofanya kila siku.
iWatch ina uwezo wa kupima miondoko ya mwili wa mtumiaji kwa ujumla hivyo kuwa kama mshauri wa karibu katika masuala ya afya ya mtumiaji na kazi mbalimbali anazozifanya.
Pia, mtumiaji anaweza kutumia Wi-Fi na GPS hivyo anaweza kupata vitu ambavyo anatumia kwenye computer yake ya (Mac) au iphone na anaweza kuchagua picha na miziki kupitia saa hiyo yenye speaker zisizoharibika kwa kuingiliwa na maji.Simu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mapema mwaka kesho na kwa mujibu wa mtandao wa ipadvisor wa Uingereza, saa hiyo itaanza kuuzwa Marekani kwa kiasi cha $349 (580,561 za Tanzania).
Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema malipo yatafanyika kwa njia/huduma mpya waliyoianzisha inaitwa ‘Apple Pay’.
Apple iWatch ina sura zaidi ya 11 na mtumiaji atakuwa na uwezo wa kubadili mikanda kadiri apendavyo.
Kampuni ya Apple mezindua pia simu zake mbili mpya ambazo ni kubwa ikilinganishwa na simu zake za awali. Screen ya iPhone 6 ina upana wa nchi 4.7 huku iPhone 6 Plus ikiwa na screen yenye nchi 5.5.
iWatch imechukuliwa kama mshindani mkubwa wa Rolex iliyokuwa imeteka soko.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!