Mtendaji mkuu wa klabu ya Liverpool Ian Ayre amepasua ukweli wa mambo baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Barwuah Balotelli.Ayre amesema baada ya kukamilisha usajili wa Balotelli akitokea Ac Milan klabu ya Liverpool ilinufaika kwa kuingia kiasi cha paund elfu 50 ambazo zilitokana na mauzo ya jezi yake ambayo ina namba 45.
Ayre amesema kiasi hicho cha pesa kilipatikana kwa siku moja, mbali na mauzo ambayo wanaendelea kuyafanya mpaka hii leo ambapo mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye maduka ya klabu hiyo.Amesema pamoja na mauzo hayo kuendelea kufanywa, uongozi wa Liverpool haukumsajili mshambuliaji huyo kwa kutaka kufanya biashara na badala yake walifanya hivyo kwa lengo la kuona soka linachezwa pamoja na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Luis Alberto Suarez Diaz aliyetimkia nchini Hispania kwenye klabu ya Barcelona.
Super Mario Barwuah Balotelli tangu aliposajiliwa na klabu ya Liverpool tayari ameshaitumikia klabu hiyo katika mchezo mmoja wa ligi ya nchini Uingereza dhidi ya Spurs na majogoo wa jiji walipata ushindi wa mabao matatu wakiwa ugenini huko White Hart Lane.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!