Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imetahadharisha juu ya uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini. Mkuu wa kamati hiyo Eric Marclay amesema kuwa, sambamba na kuongezeka utapiamlo , wakimbizi na ukosefu wa huduma za afya vimewafanya wananchi wa Sudan Kusini wataabike mara dufu na matokeo yake hali ya kibinadamu ni mbaya mno. Ameongeza kuwa, kunahitajika msaada wa haraka wa dola milioni 19 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wa nchi hiyo.
Wakati huo huo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema kuwa, kuhama malaki ya watu huko Sudan Kusini ambao wengi wao bado wanaishi kwenye kambi za muda na kusambaa baadhi yao katika maeneo ya mbali kumewafanya washindwe kufanya kazi na hivyo kuhitajia misaada. Ripoti zinasema kuwa, utapiamlo unashuhudiwa kwa wingi miongoni mwa watoto nchini Sudan Kusini.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!