Mpatanishi wa Umoja wa Afrika amesema makubaliano kati ya AU na waasi wa Sudan ni mafanikio muhimu katika jitihada za sasa za kuhitimisha mgogoro wa nchi hiyo. Thabo Mbeki rais wa zamani wa Afrika Kusini amesema hayo baada ya kuonana na Rais Omar al Bashir wa Sudan na kuongeza kuwa, kutiwa saini makubaliano kati ya AU na Harakati ya Mapinduzi ya Sudan kunahesabiwa kuwa hatua kubwa kuelekea mazungumzo ya kitaifa ya Sudan na kunaweza kuandaa mazingira ya kupatikana mafanikio makubwa zaidi.
Harakati ya Mapinduzi ya Sudan ni muungano wa makundi ya waasi wa Darfur, Kordofan Kusini na Jimbo la Blue Nile. Wiki iliyopita katika kikao kilichofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia wawakilishi wa makundi hayo waliahidi kufanya juhudi za kutatua kwa amani migogoro ya Sudan na kushiriki mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa ya nchi hiyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!