Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HIKI HAPA KILE AMBACHO SERIKALI YA MALAWI ILICHO KIAMUA KUHUSIANA NA RAIA WAKE WALIYOPO AFR/KUSINI.

HIKI HAPA KILE AMBACHO SERIKALI YA MALAWI ILICHO KIAMUA KUHUSIANA NA RAIA WAKE WALIYOPO AFR/KUSINI.

Written By Unknown on Wednesday, 15 April 2015 | Wednesday, April 15, 2015

Serikali ya Malawi imetangaza mkakati wa kuwaondoa mamia ya raia wake walioko nchini Afrika Kusini, kufuatia kuongezeka wimbi la vitendo vya chuki dhidi ya raia wa kigeni nchini humo. Taarifa kutoka Durban, Afrika Kusini zinaeleza kuwa, wimbi la chuki dhidi ya wahajiri wa kigeni limesababisha raia wanne wa kigeni kuuawa nchini humo. Wizara ya Habari ya Malawi imeeleza kuwa, kuna raia wa nchi hiyo wasiopungua 360 nchini Afrika Kusini, ambao hivi sasa wanakabiliwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya raia wa Afrika Kusini. Imeelezwa kuwa, tokea kuanza wimbi la vitendo vya chuki dhidi ya raia wa kigeni katika mji wa Durban, zaidi ya raia 1,000 wa kigeni wamewekwa kwenye kambi za muda zilizoko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi la nchi hiyo. Hadi sasa Polisi ya Afrika Kusini imeshawatia mbaroni washukiwa 50 wa mauaji hayo. Siku ya Ijumaa iliyopita, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alilaani mashambulio hayo na kusema kuwa, matatizo ya kiuchumi nchini humo hayawezi kuwa sababu ya kushambuliwa wageni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi