Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KIPIGO KIKALI CHAWAKUMBA MAJESHI YA MISRI WAKIPENYA KUINGIA YEMEN.

KIPIGO KIKALI CHAWAKUMBA MAJESHI YA MISRI WAKIPENYA KUINGIA YEMEN.

Written By Unknown on Wednesday, 15 April 2015 | Wednesday, April 15, 2015

Duru za habari nchini Yemen zimetangaza kuwa askari makumi ya Misri wameuawa na wengine kujeruhiwa katika jaribio lao la kwanza la kutaka kuingia katika eneo la Dufs lililopo kati ya mji wa Shaqrah na Aden.
Msemaji wa harakati ya Answarullah, Muhammad al-Bukhiti amethibitisha habari hiyo na kuongeza kwamba, askari hao wa Misri walifika katika eneo hilo kwa kutumia mitumbwi minne ambayo kila mmoja ulipakia askari 10. Amesema kuwa, baada ya kuingia eneo hilo, jeshi la Yemen kwa kushirikiana na wanamapambano waliokuwa wakifuatilia nyendo zao, walianza kupambana vikali na askari hao na kuua wengi miongoni mwao. Aidha amesema kuwa, askari wengine kadhaa ambao hakutaja idadi yao wametekwa nyara na wanamapambano wa Yemen. Makumi ya askari vamizi wa Saudia Arabia pia waliuawa na wengine kadhaa kukamatwa mateka katika shambulizi la kulipiza kisasi lililofanywa na wapiganaji wa kabila la Takhya Jumapili iliyopita nchini Yemen. Ripoti zinasema kuwa wanachama wa kabila la Takhya juzi Jumapili walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya kituo cha jeshi la al-Minare karibu na mpaka wa nchi hiyo na Yemen. Shambulizi hilo limefanyika kulipiza kisasi cha mauaji yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa kabila hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi