Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HUENDA STAR HUYU WA BRAZIL AKAPELEKWA JELA

HUENDA STAR HUYU WA BRAZIL AKAPELEKWA JELA

Written By Unknown on Thursday, 24 November 2016 | Thursday, November 24, 2016

Huenda Superstar wa Barcelona Neymar Jr akaenda jela kutokana na adhabu ambayo imependekezwa na mwendesha mashtaka wa Hispania baada ya mchezaji huyo wa Brazil kuhusishwa na rushwa wakati wa uhamisho wake kutokan Santos kwenda Barcelona.
Kama inavyoripotiwa na Reuters, mwendesha mashtaka ameshauri mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazil kupelekwa jela kwa miaka miwili kutokana na kuhusika kwenye kesi ya rushwa wakati wa usajili wake kutoka Santos ya Brazil kujiunga na Barca mwaka 2003.
Hata hivyo, Neymar anaweza asitumikie kifungo hicho akiwa jela kwasababu, hukumu yoyote ya miaka miwili au chini ya hapo kwa kosa la mara ya kwanza inaweza kufidiwa kwa faini kwa mujibu wa sheria za Hispania.
Sheria kama hiyo ilitumika kwa wachezaji wengine wa Barceola Javier Mascherano na Leo Messi ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi za ukwepaji wa kodi.
Neymar sio mtuhumiwa pekee kwenye kesi hiyo, rais wa zamani wa Barcelona Sandro Rosell huenda akakabiliwa na adhabu kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kutupwa jela kwa miaka mitano pamoja na faini ya dola za Marekani milioni 8.9.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi