Paulo Futre amesisitiza kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ana maadui wengi sana katika nchi yake, huku idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wakidaiwa kupenda Messi ashinde tuzo ya Ballon d’Or.
Ronaldo amejichimbia mizizi kwenye timu yake ya taifa ya Ureno na kuweka rekodi ya kipekee kwa nchi yake baada ya kuipa taji la Euro mwaka 2016.
Hata hivyo, Futre ambaye alicheza michezo 41 kwa nchi yake, anaamini kwamba Wareno wengi hawampendi Ronaldo kutokana na namna anavyojiweka katika maisha yake ya ndani na nje ya uwanja.
“Cristiano ni Mreno, amefanya kila kitu, ni bingwa wa Ulaya, lakini ana maadui wengi sana nchi Ureno kutokana na namna alivyo,” Futre alinukuliwa na SER.
“Huwa hapindishi ukweli wala hapendi kuzunguka na ndiyo maana anapata maadui wengi sana nchini mwake.. Mambo ambayo wakati mwingine huzungumza baada ya mechi na mtazamo wake ulivyo ndio tatizo kubwa sana.
“Kulikuwa na wakati watu walikuwa wanaimba Messi, Messi, Messi nje ya hoteli walikuwa wakiishi wachezaji wa timu ya Ureno, hali ambayo ilikuwa ni ya aibu mno.
“Bila shaka kuna watu nchini Ureno ambao wanataka Messi ashinde Ballon d’Or. Hiki ni kitu pekee kinachotokea Ureno.”
CRISTIANO RONALDO ANA MAADUI WENGI:PAULO FUTRE
Written By Unknown on Thursday, 24 November 2016 | Thursday, November 24, 2016
Labels:
michezo ulaya,
news
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!