Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford dakika ya saba alianza kuifungia timu yake goli moja katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
Ander Herrera dakika ya 49 aliipatia Manchester United bao la pili na kuufanya mchezo huyo kumalizika kwa Man U kushinda 2-0.
Pamoja na kufungwa, Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 75 za mechi 32 wakati United inaendelea kushika nafasi ya tano kwa pointi 60 za mechi 31.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!