Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa winga mzaliwa wa Belgium,Adnan Januzaj amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuwatumikia mabingwa hao watetezi.
Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 ambaye alianza vizuri Ligi Kuu ya Uingereza kwa kufunga goli mbili katika mchezo wake wa kwanza amejifunga kwa mashetani hao wekundu mpaka mwaka 2018.
Meneja wa Man United,David Moyes amesema kuwa amefarijika sana kuona Adnan kaamua kujifunga na kutafutia mafanikio klabuni hapo.Akidai kuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na amempa matumaini makubwa tangu awasili kuinoa klabu hiyo mwezi Julai.
![]() |
| . |
Januzaj alisisitiza kuwa ni hatua kubwa kwake kusaini Manchester United.Pia akadai tangu awasili hapo mara nyingi alikuwa akiwaza jambo hilo na kusema klabu hiyo ni chagua lake sahihi.




0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!