KLABU
ya Barcelona imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya Hispania baada ya
kulazimishwa sare ya bila kufungana na Osasuna usiku wa jana.
Huku Lionel Messi akianzia benchi, wageni walishindwa kuendeleza wimbi lao la ushindi waliloanza nalo tangu mwanzo ligi.
Neymar na Cesc Fabregas walifanya jitihada kubwa kuitafutia ushind Barca kabla ya Messi kuingia robo ya mwisho ya mchezo.
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
Lakini
Muargentina huyo hakuweza kufungua mlango wa Osasuna ambayo iliizuia
Barca kufunga bao katika ligi hiyo kwa ara ya kwanza tangu January 2012.
Real
Madrid ilipunguza pengo la pointi hadi kubaki tatu kuelekea mechi baina
yao Uwanja wa Camp Nou mwishoni mwa wiki ijayo, baada ya jana kushinda
2-0 dhidi ya Malaga Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Gareth
Bale alireea uwanjani kuichezea Los Blancos kama mchezaji wa mwisho
kutokea benchi na kusababisha penalti ambayo ilikwamishwa kimiani na
Cristiano Ronaldo kuihakikishia timu yake ushindi, baada Angel di Maria
kutangulia kufunga.
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
 |
| . |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!