Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MEMBA WA ZAMANI WA BAD BOYS ENT RAPA MASE ATANGAZA UJIO WAKE MPYA NA BONGE LA ALBUM

MEMBA WA ZAMANI WA BAD BOYS ENT RAPA MASE ATANGAZA UJIO WAKE MPYA NA BONGE LA ALBUM

Written By Unknown on Sunday, 20 October 2013 | Sunday, October 20, 2013

Rapper Mase aliyewahi kuwa chini ya Bad Boys Entertainment ameweka wazi habari muhimu kuhusu maisha yake ya muziki kwa kutangaza rasmi ujio wa album yake mpya itakayoitwa  "Now We Even". 
.
Kupitia twitter accout yake Mase ametoa taarifa hizi weekend hii na kuongezea kuwa album hii itahamasishwa na mitindo huru aliyowahi kufanya miaka kadha iliyopita pamoja na baadhi ya album za Notorious BIG Na 2 Pac ambazo amezitaja ni Life After Death Ya BIG, All Eyez On Me ya 2 Pac na Reasonable Doubt ya Jay Z.

Alivyokuwa Bad Boy Entertainment  Mase alitoa Kazi kubwa kama Harlem World ya mwaka 1997, Double Up ya mwaka 2000 na Welcome Back ya mwaka 2004. 

Baada ya kazi hizo Mase alipishana na bosi wake Puff Daddy na ndio aliacha muziki na kuwa mchungaji. Inasemekana wasanii hawa wawili sasa wanaelewana na wanafanya mpango wa kufanya kazi pamoja tena.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi