IKIWA kampeni za kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia 2014 ikifikia katika hatua tete, timu kadhaa
wiki hii zinatarajia kukata tiketi kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa
kabisa duniani. Wenyeji Brazil tayari wameungana na nchi za Japan,
Australia, Iran na Korea Kusini kwa upande wa bara la Asia huku Ulaya
kukiwa tayari na nchi za Uholanzi, Italia, Ujerumani, Ubelgiji na
Switzerland wakati Concacaf kuna timu za Marekani, Costa Rica pamoja na
wenzao wa Amerika Kusini Argentina na Colombia. Wiki hii nchi nyingine
kutoka bara la Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini na Kusini zinaweza pia
kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo. Kwa upande wa Ulaya,
Urusi inaweza kujikatia tiketi kama wakifanikiwa kuwafunga Azerbaijan
huku Ugiriki nao wakiwa na nafasi kama hiyo kama wakifanikiwa kuwafunga
Bosnia-Herzegovina wakati Uingereza na mabingwa watetezi wa michuano
hiyo nao wakiwa wamebakisha hatua moja kufikia huko. Kwa upande wa
Afrika mechi za hatua ya mtoano zitaendelea kesho ambapo Ivory Coast na
Nigeria zitajitupa uwanjani kutetea ushindi wa mechi za mkondo wa kwanza
wakati Tunisia itasafiri kuifuata Cameroon Alhamisi baada ya kutoka
sare ya bila ya kufungana mwishoni mwa wiki iliyopita.
Home »
michezo ulaya
» SAFARI ZA KUELEKEA BRAZIL ZAZIDI KUKOLEA
SAFARI ZA KUELEKEA BRAZIL ZAZIDI KUKOLEA
Written By Unknown on Wednesday, 16 October 2013 | Wednesday, October 16, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!