MTANDAO
wa wasaka vipaji wa Arsenal umepiga hatua kubwa na sasa unataka
kumsajili mshambuliaji asiyefurahia maisha Manchester United, Javier
Hernandez 'Chicharito' katika dirisha dogo la usajili Januari.
The Gunners imejadili uhamisho wa kushitua wa nyota huyo wa Mexico, kutokana na kuwa na mshambuliaji mmoja tu, Olivier Giroud.
Arsene Wenger anafahamu mapungufu ya washambuliaji aliyonayo, Giroud akiwa mtu pekee aliyenaye katika safu hiyo.
Anatakiwa: Arsenal imemuorodhesha mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez katika wachezaji inayotaka kuwasajili Januari |
Hii ni safari kuelekea Arsenal? Hernandez amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza United |
Mshambuliaji
wa Liverpool, Luis Suarez anabaki kuwa mchezaji aliye ndoto za Wenger
kumsajili, lakini Hernandez yuko juu katika orodha ya wanaoweza
kusajiliwa.
Arsenal
itajaribu kusajili mshambuliaji mpya Januari, na kumtokea kwao
Hernandez inaweza kuwa sahihi kutokana na mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 25 kutopewa nafasi kubwa ya kucheza Old Trafford.
Wenger
- ambaye pia anammezea mate mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente
anayemtaka kwa mkopo, anahofia Giroud anaweza kuumia na ndiyo maana
anataka kusajili mshambuliaji mpya Januari.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi za Arsenal katika Ligi Kuu
msimu huu pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hali inayozua hofu anaweza
kuchoka au kuumia.
Tegemeo pekee: Arsenal ina mapungufu ya washambuliaji, Olivier Giroud akiwa mtu pekee wa safu hiyo kikosini |
Wakati huo huo, Wasaka vipaji wa Gunners bado wanaendelea kumfuatilia beki wa kulia wa Monaco, Fabinho.
Mbrazil
huyo anayecheza kwa mkopo kutoka Rio Ave, amevutia katika Ligue 1 msimu
huu, na kiwango chake kimemkuna Msaka vipaji wa Arsenal aliye Ufaransa,
Giles Grimandi. Wenger amewaambia wachunguzi wake kumtambulisha beki
mpya wa kulia akihofia mustakabali wa muda mrefu wa Bacary Sagna katika
klabu hiyo.
Mfaransa huyo hafiksihi mwaka katika Mkataba wake aliobakiza na bado anasuasua kusaini Mkataba mpya.
Bado inamtolea macho: Wasaka vipaji wa Arsenal wanamfuatilia beki wa kulia wa Monaco, Fabinho |
Makinda
wenye vipaji wa Brazil, Boschilia na Nathan - ambao wamefunga mabao 11
baina yao katika Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17
Falme za Kiarabu (UAE) pia wameivutia The Gunners.
Msaka
vipaji Mkuu, Steve Rowley amewatazama wawili hao katika michuano hiyo,
na wasaka vipaji wataendelea kufuatilia maendeleo yao. Mshambuliaji wa
Standard Liege, Michy Batshuayi, pia yupo kwenye rada za Arsenal.
Msaka
vipa wa Ulaya, Ty Gooden amekuwa akimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo
wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ubelgiji, ambaye
amefunga mabao 14 msimu huu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!