PAMOJA na kuwa kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara, straika wa Simba, Amissi Tambwe, amesema hajaridhishwa na kiwango alichokionyesha kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
Tambwe anacheza ligi hiyo mara ya kwanza na ndiye kinara wa mabao akiwa na mabao tisa kabla ya mechi ya jana Jumatano.
Wanaomfuatia ni Hamis Kiiza wa Yanga (manane),
Muivory Coast Kipre Tchetche (Azam FC), Juma Luizio (Mtibwa Sugar) na
Elius Maguli (Ruvu Shooting) wote wamefunga mara saba.
Tambwe alisema:
“Sijaridhika na kiwango nilichocheza mzunguko wa kwanza. Malengo yangu
ni kuifanyia makubwa zaidi Simba. Nilipokuwa Burundi nilimaliza mzunguko
kama huu nikiwa na mabao 15, lakini hapa sijafanikiwa.”
Tambwe mfungaji bora wa Ligi Kuu Burundi msimu
uliopita akiwa na mabao 21 na Kombe la Kagame alipofunga sita, alisema:
“Lakini pia, timu yangu haijafikia malengo, nilitaka twende mapumziko
tukiwa tunaongoza ligi jambo ambalo nafikiri kwetu, limeshindikana.
“Hata hivyo, silalamiki sana kwasababu ni ugeni,
unajua hapa si sawa na kule kwetu, bado sijaizoea lakini pia nimekutana
na wachezaji wapya naamini mzunguko wa pili, tutakuwa tumekaa pamoja
kipindi kirefu na kuzoeana, hapo mambo yatapokuwa mazuri.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!