Kimbunga kikali kiitwacho “Super typhoon Hayan” kinachokadiriwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kimeanza kuipiga Ufilipino kikiwa kimeandamana na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya karibu kilomita 300 kwa saa na kusababisha mawimbi ya bahari kwenda juu urefu wa mita 15 katika maeneo ya pwani.
Wataalam wa hali ya hewa wanasema iwapo makadirio ya mwanzo yaliyozingatia picha za satelaiti yatakuwa hivyo basi kimbunga hicho kitakuwa kikubwa kuliko vyote kuwahi kutokea katika nchi hiyo ambako shule na maofisi vimefungwa kuepuka madhara huku maelfu ya watu wakihamishwa kutoka maeneo yanayohofiwa kukumbwa na kimbunga hicho.
. |
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!