Wananchi wa Afrika Kusini hii leo wanaanza kushiriki zoezi la
usajili wa wapiga kura litakalofanyika kwa siku mbili mfululizo, ikiwa
ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2014 ambao unaenda sambamba
na maadhimisho ya miaka ishirini tangu kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi.
Rais wa Taifa hilo Jacob Zuma amewataka raia wake kujitokeza
kwa wingi katika zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika kwa amani na
utulivu, huku vyombo vya usalama vikisema vimejidhatiti kuhakikisha
hakuna uvunjifu wowote wa amani utakaojitokeza.
Vijana waliozaliwa baada ya mwaka 1994 ambao kwa mara ya kwanza washiriki zoezi hilo baada ya kutimiza umri unaoruhusiwa, wamehimizwa kujitokeza zaidi na kuchaguzi viongozi wao.
Zuma ambaye anatarajiwa kuwania tena Urais katika uchaguzi ujao kupitia chama tawala cha ANC amesema anatarajia uchaguzi ujao utaendeleza historia nzuri katika utawala wa kidemokrasia ndani ya Taifa hilo.
Hata hivyo umaarufu wa kiongozi huyo na chama chake kilichokumbwa na migogoro na utadhihirika hapo mwakani atakapochuana na Julius Malema ambaye alitimuliwa kutoka katika chama hicho.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!