Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho hajakubali msamaha kutoka kwa nyota wa klabu hiyo Eden Hazard mara baada ya kukosa mazoezi ya timu hiyo siku chache zilizopita.
Hazard alishindwa kuhudhuria mazoezi katika klabu yake ya Chelsea hivyo aliachwa nje ya kikosi kilichoshinda mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Shalke.
Mreno huyo licha kutokubali msamaha huo amedai kuwa kutompanga nyota huyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza Jumamosi dhidi ya West Brom ni sawa na kujitoa muhanga.
Huku akikiri kuwa Hazard alikwisha omba msamaha kwake na kwa klabu pia ila ingawa msamaha ni kama haujakubaliwa ila jambo hilo limekwisha na cha msingi kuangalia mbele.
Pia akasema kuwa amechaguliwa katika kikosi kitakachoshuka Stamford Bridge leo na yupo tayari kucheza kwa hali kubwa.Huku akiongeza kuwa ukiwa kama meneja mara nyingine inatakiwa ufanye maamuzi magumu.
Raia huyo wa Ubelgiji alikwenda nchini Ufaransa kutazama mchezo wa Ligue 1 kati ya klabu yake ya zamani ya Lille dhidi ya Monaco siku ya Jumapili Usiku na akashindwa kufika katika uwanja wa Cobham ambapo klabu yake ya Chelsea ilikuwa ikifanya mazoezi siku ya Jumatatu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!