Mapambano makali baina ya makabila mawili katika eneo la Gedo Barkan karibu na Jowhar yamesababisha mauaji ya watu wapatao18 na wengine 20 kujeruhiwa kutoka Alhamisi (tarehe 7 Novemba), Garowe Online wa Somalia uliripoti.
Makabila hayo mawili yaliripotiwa kuwa na mapambano Jumatano kufuatia mabishano kuhusu umiliki wa ardhi ya kilimo.
Mgogoro huo kisha uliendelea Alhamisi wakati wakaazi waliporipoti wanaume wenye silaha kupiga risasi kwenye shamba la kilimo na nyumba.
Mapambano hayo yamekuja baada ya Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kuzuru mji wa Jowhar kukagua uharibifu wa mafuriko ya hivi karibuni.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!