Msemaji rasmi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini
Somalia AMISOM, ametangaza kushadidisha mashambulizi yake dhidi ya kundi
la ash-Shabab na waungaji mkono wake katika maeneo ya kusini mwa
Somalia.Ali Aden Houmud ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa
habari mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia na kuongeza kuwa, vikosi vya
AMISOM vimekusudia katika siku zijazo kuanzisha operesheni kali kwa
ajili ya kulitokomeza kundi hilo la ash-Shabab. Amesema, operesheni hizo
zitajikita zaidi katika maeneo ambayo yanatajwa kutumiwa na kundi hilo
kwa ajili ya kuendeshea harakati zake. Aidha Msemaji huyo rasmi wa
vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM
ameonyesha kusikitishwa kwake na vita vya kikabila vinavyoendelea huko
katika jimbo la Shabeellaha katikati mwa Somalia na kusisitizia juu ya
udharura wa kurejeshwa hali ya usalama na amani baada ya miaka mingi ya
vita na uharibifu mkubwa ambao umekuwa ukifanywa na makundi ya wabeba
silaha nchini humo. Hii ni katika hali ambayo mji wa Mogadishu nao
umekuwa ukishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na
wapiganaji wa ash-Shabab dhidi ya raia na viongozi wa serikali.
Home »
siasa afrika
» AMISOM YATANGAZA KUANZISHA MASHAMBULIZI MAPYA NCHINI SOMALIA
AMISOM YATANGAZA KUANZISHA MASHAMBULIZI MAPYA NCHINI SOMALIA
Written By Unknown on Sunday, 29 December 2013 | Sunday, December 29, 2013
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!