Afisa mwandamizi mmoja katika Wizara ya Mafuta nchini Libya, amesema
kuwa serikali ya Tripoli itaanza kusafirisha mafuta yake kupitia bandari
ya Al Hariqa mashariki mwa nchi hiyo siku chache zijazo. Hatua hiyo
inakuja baada ya kufikiwa makubaliano kati ya serikali na makundi ya
wabeba silaha wanaoendelea kuzizingira bandari za kusafirishia mafuta za
nchi hiyo. Kwa mujibu wa habari, watu hao wenye silaha walichukua hatua
ya kuzingira bandari hiyo ya Al Hariqa tangu mwezi Agosti mwaka huu
2013 kwa shabaha ya kuishinikiza serikali ya Tripoli kuweza kutekeleza
matakwa yao ya kisiasa na kifedha. Hata hivyo juhudi za serikali ya
Libya kwa ajili ya kumaliza mzingiro huo dhidi ya bandari za
kusafirishia mafuta, zimekuwa zikigonga mwamba na hivyo kutishia uchumi
wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Wiki iliyopita umoja wa
wafanyakazi wa mafuta na gesi nchini Libya, ulitangaza kwamba, kuna
uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya wapinzani na serikali ya nchi
hiyo kuhusiana na mgogoro wa kufungwa bandari za mafuta, ulioanza tangu
miezi kadhaa iliyopita. Hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu uzalishaji
wa mafuta nchini humo ulikuwa umefikia kiwango cha pipa laki mbili na 24
elfu kwa siku huku kikiwa kimepungua mara dufu hadi sasa.
Home »
siasa afrika
» SERIKALI YA LIBYA YAFIKIRIA KUANZA MPANGO WA KUSAFIRISHA MAFUTA KUPITIA BANDARI YA AL-HARIQA
SERIKALI YA LIBYA YAFIKIRIA KUANZA MPANGO WA KUSAFIRISHA MAFUTA KUPITIA BANDARI YA AL-HARIQA
Written By Unknown on Sunday, 29 December 2013 | Sunday, December 29, 2013
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!