KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, anaamini kuwa huu ni wakati wa
kuachana na bao la ugenini katika michuano yote inayoandaliwa na
Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) huku akisema kuwa bao hilo halitendi
haki.
Wenger alikuwa akijadiliana na makocha wenzake
jijini Geneva huku akitolea mfano wa pambano la mtoano la Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu uliopita dhidi ya Bayern Munich ambapo walitoka
sare ya 3-3 lakini bado Bayern Munich ikasonga mbele.
“Mwaka jana tulitolewa kwa mabao ya ugenini na
baada ya hapo niliwaomba Uefa waachane na sheria hii. Ona, kwa mfano
tulifungwa mabao 3-1 nyumbani lakini tukashinda 2-0 ugenini. Ni vigumu
kucheza na Bayern halafu usiruhusu bao. Nguvu ya bao la ugenini imekuwa
kubwa sana,” alisema kocha huyo Mfaransa.
Arsenal imepangiwa kucheza mechi mbili za mtoano
kwa mara nyingine na Bayern Munich wakati michuano ya mwaka huu
itakapoendelea Februari na Machi mwakani.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!