Msanii wa R&B, Ben Pol kutoka nchini Tanzania ameelezea maendeleo ya utafiti wa muziki wa asili aliouanza mwezi December mjini Dodoma.
Ben Pol amesema kuwa tayari ameshafanya maandalizi yanayohitajika lakini bado hajazama ndani kuanza kuufanya utafiti huo.
Amesema amerudi Dar es Salaam wiki iliyopita kwa kuwa alikuwa na show ijumaa (December 20), lakini pia anamalizia project ya wimbo wake ambao atauachia January mwakani.
“Project ya January ni single mpya kwa ajili ya mwaka mpya na natarajia kuuachia katikati ya January. Bado sijaipa jina, na bado sijafikiria kumshirikisha mtu lakini hadi sasa kuna back up za wasichana na nini…akina Alice.” Ben Pol amesema.
Amefunguka kuwa mdundo wa wimbo huo umetayarishwa na Fundi Samweli aliyeko nchini Sweden na vocal zinafanywa na Imma The Boy.
Maneno Maneno hit maker amesema kuwa ataendelea na utafiti wake lakini pia ataendelea kufanya shows kama kawaida hasa siku za weekend .
“Utafiti wangu lazima uendelee, kwa mfano weekdays jumatatu, jumanne jumatano, alhamisi na ijumaa, hizo zote ni siku ambazo zinanitosha sana ukitoa weekend ambazo ndio zinakuwaga zinashows.” Amesema Ben Pol.
“Kwa hiyo tutaenda hivyo, hatuwezi tukasitisha shows kabisa kwa sababu inabidi tukidhi mahitaji ya watu, watu wanataka shows na burudani kwa hiyo ni lazima tuwafikie.”

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!