Mashabiki wa soka duniani watanyimwa raha ya macho baada ya mwanamitindo
kutoka nchini Brazil, Fernanda Lima kusema atavaa nguo ya kufunika
zaidi wakati wa tuzo za FIFA Ballon d'Or Januari mwakani.
Fernanda mwenye umri wa miaka 36 alipata umaarufu duniani baada ya kuongoza droo ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 iliyofanyika mjini Costo do Sauipe,Brazil.Hata hivyo mrembo huyo amelazimika kubadilisha kivazi chake kwa sherehe za utoaji wa tuzo za Ballon d'Or mjini Zurich,Uswizi Januari 13.
Hii ni baada ya kupata maelfu ya malalamishi kutoa kwa raia wa Iran baada ya wakurugenzi wa kituo kimoja cha televisheni nchini humo kukatiza matangazo hayo kutokana na muonekano wake kuwa wa kuwamezesha watu mate.Aidha Fernanda ameomba radhi kutokana na kivazi hicho na kusema si nia yake kukosea nchi yoyote,utamaduni,watu au kuzua utata.Wanasoka Lionel Messi(Barcelona), Franck Ribery(Bayern Munich) na Cristiano Ronaldo(Real Madrid) ndio wanaowania tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa mwaka duniani.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!