Ripoti zinaeleza kuwa mashambulizi dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yameshadidi hasa katika mji mkuu Bangui, huku wafuasi wa dini hiyo ambao ni wachache wakiendelea kulengwa na mashambulizi ya kulipiza kisasi. Wanamgambo wa Kikristo wanaoitwa Anti Balaka wanawashambulia Waislamu na hata kuchoma misikiti na mali zao ili kulipiza kisasi cha mashambulizi ya huko nyuma ya waasi wa Seleka.
Hayo yanajiri huku askari wa Ufaransa wakiwepo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na inadaiwa kuwa askari hao wanawaunga mkono wanamgambo wa Kikristo. Imearifiwa kuwa, katika siku za hivi karibuni wanajeshi wa Ufaransa walioko Bangui wamewatimua wanamgambo Waislamu wa kundi la Seleka na hivyo kuwaacha raia Waislamu bila ulinzi.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, katika miezi 10 iliyopita zaidi ya watu elfu 2 wamepoteza maisha yao katika machafuko ya nchi hiyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!